Usharika wetu ni "Usharika WaKimasihi unaoshika Torati" ukihusisha wale waliozaliwa kama Wayahudi na wale wa mataifa, walio pandikizwa katika jumuiya ya Israeli, kwa kumpokea Yeshua kama Masihi wao (Waefeso 2:12-13).
Tunaamini Yeshua ni Torati hai aliyekuja kutimiza Torati kwa uaminifu na siyo kuitangua. Torati ni hai na nzima, inaishi katika mioyo ya wote wamuaminio.
Kwa hiyo uchaji wake siyo hiari bali ni uhitaji kwa wote wanaodhamiria kumfuata Mashiach (Masihi) wetu, ambaye baada ya kutimiza Torati kwa ajili yetu, alilipa gharama (Asham - sadaka) ya makosa yetu, hivyo akatangua katika mwili Wake madhara ya kutokutii kwetu (dhambi na mauti). Tunakazana kutembea katika njia Zake kwa sababu tunampenda. Tunaamini kwamba Torati na neema zinaishi pamoja leo, nasi tunahitaji kutimiza Sheria za MUNGU na Neema ya MUNGU inatusamehe wakati tumejaribu na kushindwa.
Tukiwa ni usharika wenye uchaji wa Torati inamaanisha kwamba tunafundisha na kuhimiza wanachama na wafuasi kujizoesha na Torati majumbani mwao na kama maisha ya uadilifu kwa ujumla. Hii inamaanisha vilevile kusherekea moedim (sherehe) zote za Kibiblia kama inavostahili na kwa siku zilizoamriwa. Kuwa na uchaji wa Torati ina maana tunaheshimu siku ya Shabati na kuacha kufanya kazi zozote pamoja na kutokununua na kuuza, kuanzia machweo ya Ijumaa hadi machweo ya Siku ya Saba (Jumamosi).
Uchaji wetu wa Torati unaendelea hadi katika muundo wetu na taratibu za ibada. Ingawa sisi ni Wakarisimatiki (tunaamini katika vipawa na kazi za Ruach HaKodesh [Roho Mtakatifu]), bado tunapendelea zaidi muundo wa ibada ya kiasili. Shabati inaanza na ibada ya Erev Shabati "Kabalah Shabati" (kukaribisha Shabati), imbayo inahusisha litrugia, kusifu na kuabudu na kujifunza Torati kwa kujadiliana . Ibada za Shabati zinaanza saa 3.00 asubuhi ya Siku ya Saba (jumamosi), pamoja na saa moja na nusu ya kujifunza Torati ya parasha ya wiki (masoma ya wiki ya Torati).
Ibada za kawaida zinaanza saa 5:00 asb. Na kuchukua kama masaa matatu. Ibada hii inaanza na litrugia na kuendelea na maombi, sifa na kuabudu Kimasihi (pamoja na dansi ya Kidaudi), ibada ya Torati ya kiasili yenye ufasihi, D'var Torah (tafakari ya masomo ya kila wiki), na kumalizia na mahubiri ya Rabbi. Ingawa hii ni ibada ya kawaida, haimaanishi kwamba tumeambatana nayo kimadhubuti. Uongozi unaruhusiwa kugeuza ibada na yale yaliyomo, kama vile watakavyoongozwa na Ruach HaKodesh.
Sisi hapa Melech Yisrael tunajihesabia zaidi ya usharika; sisi ni jamii hai inayojishughulisha ya waamini wa Masihi, tukiwa na ibada mbalimbali na mashughuliko yanayotendeka wiki nzima. Upekee wetu unatokana na kwamba sisi sote tunatokana na wale ambao ni Wayahudi na wasiyo Wayaahudi, tumeunganishwa pamoja katika kumuabudu Masihi wetu katika desturi na mila za Torati, wakati huohuo tukithibitisha uweza na uhuru wa Ruach HaKodesh.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
huh? I not understand
Post a Comment